Matthew 24:45-51

Mfano Wa Mtumishi Mwaminifu

(Luka 12:41-48)

45 a “Ni nani basi aliye mtumishi mwaminifu na mwenye busara, ambaye bwana wake amemweka kusimamia watumishi wengine katika nyumba yake, ili awape chakula chao kwa wakati unaofaa? 46 bHeri mtumishi yule ambaye bwana wake atakaporudi atamkuta akifanya hivyo. 47 cAmin, nawaambia, atamweka mtumishi huyo kuwa msimamizi wa mali yake yote. 48 dLakini kama huyo mtumishi ni mwovu, naye akasema moyoni mwake, ‘Bwana wangu atakawia muda mrefu,’ 49 ekisha akaanza kuwapiga watumishi wenzake, na kula na kunywa pamoja na walevi. 50Basi bwana wa mtumishi huyo atakuja siku asiyodhani na saa asiyoijua. 51 fAtamkata vipande vipande na kumweka katika sehemu moja pamoja na wanafiki, mahali ambako kutakuwa ni kulia na kusaga meno.

Copyright information for SwhNEN